INATUPASA KUUTUMIA VEMA #WAKATI ❗ Hivi sasa, ni zaidi kidogo ya miezi miwili, tangu tuliposherehekea #Christmas na baadaye Mwaka Mpya wa 2019. Je, unakumbuka ulimwambia nini Mungu katika #maombi yako, muda mfupi kabla ya kumaliza mwaka 2018, na kuingia mwaka mpya wa 2019❓ Je, wewe ulikuwa miongoni mwa #wapendwa waliomwahidi Mungu kwamba, mwaka huu watamtumikia Mungu kwa ari na juhudi kubwa, na kufanya kila wawezalo kulifanya, ili kumzalia Mungu matunda, na kuhakikisha #matunda hayo yanakaa (YOHANA 15:16)❔ Je, mpaka sasa umetekeleza #ahadi yako kwa kiasi gani❓ Kumbuka, Ndiyo yetu ni lazima iwe Ndiyo, tena haipendezi mbele za #Mungu, kumwambia uongo Roho Mtakatifu (2 WAKORINTHO 1:17-18; MATENDO 5:1-11). Saa ya kuamka katika usingizi imewadia❗(WARUMI 13:11). Inatupasa kuutumia vema ( #kuukomboa) wakati, maana zamani hizi ni za uovu! (WAEFESO 5:16). . . . . Chanzo cha bandiko hili ni Baba askofu mkuu Zachary #Kakobe kurasa ya #Facebook hii https://www.facebook.com/342053105875881/posts/2114705351943972/ https://www.instagram.com/kongwastone/p/BvBp6kxlJW5/?utm_source=ig_tumblr_share&igshid=19vtbtanfudez