Hadi lini, nitalia, kuchao nikiteseka, Hadi lini, n'tashangaa, watu wakiimarika, Hadi lini, tangalia, nikose kusaidika, Hadi lini, duniani, majuto yataniisha? ~Utunzi wa Hosea Namachanja #Mwanagenzi
Hadi lini, nitalia, kuchao nikiteseka,
Hadi lini, n’tashangaa, watu wakiimarika,
Hadi lini, tangalia, nikose kusaidika,
Hadi lini, duniani, majuto yataniisha?
Hadi lini, maishani, nitakosa hangaiko,
Hadi lini, masomoni, vitanikwepa vituko,
Hadi lini, safarini, ntaona mteremko,
Hadi lini, duniani, majuto yataniisha?
Hadi lini, tajikuta, nimeipata ajira,
Hadi lini, nitateta, nisipatwe na hasira,
Had…