Kuna vita kati ya hisia na mantiki na mara nyingi hisia hushinda, lakini kushinda hisia lazima utumie hisia nyingine. Kutumia hisia kushinda hisia ni kujiandaa kisaikolojia! Kwa mfano, unapokuwa unasubiria matokeo ya mtihani wako wa mwisho, kutakuwa na vita kali sana akilini mwako kati ya hisia na mantiki. Hisia itataka ushindwe au ushinde, lakini mantiki itataka ushinde au ushindwe, kutegemeana na jambo unalolitarajia. Ukitaka mantiki ishinde itakubidi utumie hisia nyingine, itakayokuwa kinyume na ile hisia ya kwanza, kuwa sawa na mantiki. Yaani, kama mantiki ni "nitashinda", hisia ya kwanza itakuwa "sitashinda"; na hisia nyingine itakuwa "sitashindwa", ambayo ni sawa mantiki. Au, kama mantiki ni "nitashindwa" (labda kwa kuwa huna vigezo vya hicho unachokitarajia), hisia ya kwanza itakuwa "nitashinda" (labda kwa kutegemea neema ya Mungu); na hisia nyingine itakuwa "nitashindwa", ambayo ni sawa na mantiki. Kwa hiyo, kama unahisi utashindwa mtihani wako jiandae mapema akilini mwako kupokea matokeo ya aina yoyote ile utakayoyapata. Vilevile, kama unahisi utashinda mtihani wako jiandae mapema akilini mwako kupokea matokeo ya aina yoyote ile utakayoyapata. Yaani, kuwa na mpango mbadala endapo mpango unaoutegemea utashindikana au utafanikiwa kwani, kushindwa au kushinda kunategemeana na nguvu ya Mungu. Kama utashindwa, sawa, mshukuru Mungu. Kama utashinda, sawa, mshukuru Mungu pia! Hivyo ndivyo unavyoishinda hisia. Yaani, hisia ya kwanza inapokuwa hasi, hisia ya pili lazima iwe chanya. Hisia ya pili inapokuwa chanya maana yake ni kwamba umeruhusu maisha yako yaendelee bila kujali aina ya jibu utakalolipata. Yaani, hisia unaishinda kwa kufikiria chanya kuhusu jambo lolote unalolitarajia! Fikiria kuwa wewe ni mshindi hata kama hisia itakwambia tofauti. Fikiria kuwa wewe ni mtakatifu hata kama hisia itakwambia kuwa wewe ni mwenye dhambi. Lakini usiache kusali, kwani bila kusali utafanikiwa kwa "private Providance" (utafanikiwa kwa neema ya Mungu). Fikiria kabla ya kutenda; kisha, ukishatenda, fikiria chanya baada ya kufikiria. Tumia hisia mbadala ili ufikirie sawasawa na mantiki yako. #hisia #emotion #mantiki #logic #neemayamungu #privateprovidence https://www.instagram.com/p/Bs39u6Nn-bG/?utm_source=ig_tumblr_share&igshid=152ma9tltvep4