Viungo Ukinikata
Hili ni suala tata, runinga magazetini, Mautini wanatweta, kupokonywa za mwilini, Hili limeshakita, twabaki wazi vinywani, Viungo ukinikata, vitakufaidi nini? Nifapo unanifata, kisu chako mfukoni, Viungo unanivuta, uviondoe mwilini, Viungo vitafukuta, japo nimo mautini, Viungo ukinikata, vitakufaidi nini? Mungu atakufufuta, jizi atakulaani, Wewe umekula mwata, kwa wafao u muhuni, Shida…

















