Repost from @cloudsfmtz #WanaotakiwaKutupongezaHawaoniKamaTunahitimu. . #RugeMutahaba anasema kwamba mamlaka yoyote na watu binafsi wanaoona #TigoFiesta ni tukio la siku moja wanakosea. "Kama wao wanaona ni tukio la siku moja wanakosea kwa sababu kuna watu wanajua hii ni movement ya miaka mingi. Ndio maana malegendary kama kina Afande Sele wanatoka Morogoro kuja huku kwa sababu wanajua tulipotoka na kufika hapa inapaswa kuwa sherehe kwa kila mpenda burudani. Tumehangaika sana miaka mingi tukiamini kuna siku tutahitimu, siku ya kuhitimu imefika wanaopaswa watupongeze wanatuvuta nyuma" #RugeMutahaba amesisitiza kwamba tulitarajia kuona Serikali na kila mtu ikiunga mkono tukio hili kubwa ambalo tumesubiri kwa miaka mingi lakini tunakutana na vikwazo vingi. #TigoFiesta2017: Mtanzania utachagua kuhitimu na wasanii wetu au utaipuuza heshima ya muziki wetu?













