MANENO YA MZEE WETU KALIKAWE. . . Namkumbuka Mzee Kalikawe wa Kunduchi. Yeye alikuwepo mwisho wa miaka ya 90 tukifanya Summer Jam. Alikuwepo pia miaka ya 2000 mwanzoni kabisa, #SummerJam ilipobadilika na kuwa Fiesta, na vilevile alikuwepo 2004 tulipokuwa tunapiga Fiesta kwenye mikoa 3 tu na mzigo ulikuwa unapigwa asubuhi. . Mzee Kalikawe aliona ugumu wa mazingira ya wakati ule, Muziki ulikuwa haupewi heshima, hatukuwa na matamasha na riziki haikuwa kubwa kama leo. Mzee Kalikawe alitutia moyo, alikutukumbusha kwamba lengo ni kuinua muziki wetu, alitukumbusha jukumu letu la kuzalisha mastaa kwa ajili ya Taifa hili. Hayo yalitokea, ndani miaka yote #TigoFiesta imekuwa tamasha kubwa zaidi, tumefanya kazi usiku na mchana, kuna vijana wengi tumewatoa machakani na kuwapa majina makubwa, tumejenga heshima ya muziki na kutengeza fursa milioni za watu kupata riziki. . Hayo hayakutufanya tunyanyue mabega na kujisifu na hata mzee Kalikawe alituasa kwamba "Ninyi ni watumishi wa Tanzania, hii kazi tuliwatuma na tunafahamu mtaendelea kuifanya. Msisahau kuwa Mnyenyekevu na muendelee kutumikia watu" . Kwa #VibeKamaLoteeeee sisi tunamshukuru Mzee Kalikawe na Watanzania wote wanaozidi kuwa nasi kila siku. #TigoFiesta2018 @tigo_tanzania @tatumzuka https://www.instagram.com/p/BqdBdG7hX4C/?utm_source=ig_tumblr_share&igshid=1eql60g5cqjzv












