Gharama katika kusafiri ni jambo lisiloepukika, lakini ukweli nikwamba kusafiri sehemu mbalimbali kuna faida kubwa sana. Kama ulishawahi kusikia faida za kusafiri basi ongeza na hizi nondo muhimu kutoka kwa @modealertz . 1. Kusafiri huongeza uzoefu wa kujifunza mambo mapya kuhusu tabia, tamaduni na mtindo wa maisha wa watu wa jamii zingine. 2. Kusafiri sehemu mbalimbali huongeza uwezo wa mtu kuibua vipaji ambavyo vimejificha ndani yake hata hivyo kusafiri huongeza uwezo wa ubunifu wa mtu . 3. Kubwa zaidi nikwamba kusafiri sehemu mbalimbali hutanua wigo wa fursa za kimaendeleo , kuongeza idadi ya washirika wa kibiashara na uwekezaji. Zingatio: Unashauriwa kusafiri kwasababu maalumu ikiwa kifedha hupo vizuri. Wale wazee wa kuhangaika na nchi za watu hizo picha ni wapi hapo? #dailymodealer #modealertv #modealer839 #followme https://www.instagram.com/p/ClPKVbPKG3k/?igshid=NGJjMDIxMWI=









