HABARI KUTOKA TANZANIA - APNAC IMEJADILI JINSI YA KUPAMBANA NA RUSHWA KWENYE VIPIMO VYA MAZAO Hayo ameyasema leo jijini Dodoma alipokuwa akifungua Semina ya wabunge juu ya changamoto na mafanikio ya sheria ya vipimo ikiwa ni pamoja na wabunge hao kutoa michango yao katika semina hiyo jinsi ya kupambana na rushwa katika vipimo. Wabunge hao ni wanachama wa hiari wa chama cha kupambana na vitendo vya rushwa APNAC ambao hutoa michango juu ya kupambana na rushwa na kuifikisha panapo husika. Spika amesema kuwa wakulima wamekuwa wakinyonywa sana na baadhi ya wafanyabisha kwa kutumia vipimo ambavyo si sahihi ikiwemo ufungaji wa mazao kwa njia ya lumbesa. “Rasilimali nyingi zimekuwa zikipotea kutokana na ufungashaji kwa njia ya lumbesa , na nyinginezo ambazo si rasmi tufikie wakati tuwe na sheria kali zaidi kwani wakulima wetu wamenyonywa na kupunjwa vya kutosha” amesema Ndugai Akitolea ufafanuzi kuhusiana na vipimo vya magari ya mizigo Spika alishangazwa kuona kuwa magari hayo licha ya kupita katika mizani mbalimbali lakini bado yanzuiwa sehemu Fulani kwa sababu ya kutakiwa kupimwa tena. Aidha amesema kuwa hali hiyo imekuwa ikiwakera wananchi kwani hawaelewi nini tatizo mpaka kuwepo kwa vipimo kila sehemu na kufanya msururu wa magari kuwa mkubwa kusubiri kupimwa. “Kama ni magari ya mizigo inawezekana wakaongeza njiani lakini kama wale wanaosafirisha mafuta kweli jamani tuliangalie na hilo tuliangalie” amesisitiza Spika Ndugai amesema kuwa hali hiyo ni chimbuko la rushwa kwani kama mfanyabishara anayesafirisha mafuta ameshapima vituo vyote hakuna sababu ya kumzuiakwani uwezekano wa kuongeza ujazo wa mafuta njiani ni mdogo. Kwa upande wa vipimo, Waziri wa Biashara na Viwanda, Joseph Kakunda amesema kuwa bado kuna changamoto kubwa katika suala la vipimo. #viwanda #ndugai #apnac #rushwa #corruption #sdg #goal16 #tanzania #africa #parliament #industrial https://www.instagram.com/p/BtHO0C_BPNM/?utm_source=ig_tumblr_share&igshid=o3l5kniwslh9















