UGONJWA WA SURUA ā Surua āāmeaslesāā ni ugonjwa unaoweza kuambukizwa kwa urahisi sana, na ulikuwa ugonjwa uliowapata watoto wengi sana kabla ya enzi ya chanjo kuanza. ā Inaweza kuchukua mpaka siku 10 kabla ya dalili kuonekana baada ya kuambukizwa. Mwanzoni mtoto anapatwa naĀ kikohoziĀ kikavu, kuchuruzika makamasi, macho yakuwa mekundu na baadaeĀ homa. ā Baada ya siku 2 ā 4, madoadoa mekundu au kahawia hujiokeza usoni na baadae kusambaa miguuni na mwili mzima. Kunaweza kuwepo madoa meupe kwenye sehemu ya ndani ya mashavu. ā Watoto wengi hupona vizuri tu. Lakini surua inaweza kusababishaĀ maambukizi sikioniĀ na matatizo mengine kama vile homa ya mapafu na kwa mara chache kuvimba ubongo. ā” JIFUNZE ZAIDI HAPA( BIO) šhttps://wikielimu.com/ugonjwa-wa-surua/ #wikielimu #afya #surua https://www.instagram.com/p/CN60JmfLYeA/?igshid=1a1p0eetsa7vx













