Bastola ya Panthera Tigrisi aliyoipenda zaidi kuliko zote iitwayo Sig Sauer P220, tamka ‘Sig Sawa’ P220, aliyojilindia dhidi ya Vijana wa Tume na watu wengine huko Oaxaca na Mexico City nchini Meksiko. Licha ya pete kubwa ya dhahabu na kidani kidogo cha almasi kwenye pete hiyo katika mkono wake wa kulia kwa ajili ya unajimu; alama nyingine kubwa ya Panthera Tigrisi ni bastola ya Kijerumani ya SIG Sauer na bunduki ya Kirusi ya AK-47 au Kalashnikov, ijulikanayo huko Meksiko kama ‘cuerno de chivos’ au ‘mapembe ya mbuzi’ kwa lugha ya Kiswahili; huku walinzi wake wakitembea na bunduki fupi nene za Kibelgiji, zenye uwezo wa kutoboa kinga ya risasi, za FNP90 (‘mata policias’ au ‘kiboko cha polisi’ kwa tafsiri ya Kiswahili. Popote ‘Jefe de Jefes’ (Bosi wa Mabosi) alipokwenda alitembea na silaha hizo, hata kanisani huko Oaxaca na Sinaloa. Enock Maregesi, mwandishi wa Kolonia Santita #sigsauer #sigsauerp220 #fnp90 #cuernodechivos #jefedejefes #ak47 #kalashnikov https://www.instagram.com/p/BtlTxagHEd-/?utm_source=ig_tumblr_share&igshid=15weibw9tslo9