Mwili wa binadamu unabadilika kutokana na mambo mengi. Hakuna anayependa unene (inawezekana wapo). Wakati mwingine unanenepa sio tu sababu ya kula kama wengi wanavyofikiri. Yapo mambo mengi yanayofanya mtu kunenepa. Stress, maradhi, dawa, umri Na hata mambo usiyofikiria. Nimepambana na unene kwa zaidi ya miaka 15! Nimetamani sana kuwa na six packs, lakini sikufanikiwa. Watu walinikejeli kwa unene. Ukiweza picha unaambiwa “tumbo hilo” hawaoni kingine. Unapambana unapungua kiasi. Badala ya pongezi unaulizwa “vipi mbona umepungua sana, unaumwa?”! Sijui iweje. Tuwahurumie wenye miili yenye shukrani kupitiliza. Tusiwakejeli wanene, hatupendi unene, ila the “struggle is real”! Kama wewe unaweza kufanya diet au mazoezi ukapungua, shukuru. Be nice, usimkejeli mtu mnene, huwezi kujua anapitia nini. Mshauri na si vibaya ukakaa kimya kama huwezi kusema maneno ya faraja. #mtotowanesi #unene #powerbreakfast #hatupendiunene #unenesiugonjwa (at Morogoro) https://www.instagram.com/p/CTQ2_4QCGEn/?utm_medium=tumblr













