Kilio cha Mkulima
Nawatafuta mafundi, wajuzi wa hii fani, Shamba langu la mahindi, limevamiwa na nyani, Wanakuja kwa makundi, tena wazi hadharani, Mkulima nina tabu, shamba kavamia nyani. ~Utunzi wa Kinyafu Marcos #Mwanagenzi
Shairi~KILIO CHA MKULIMA
Nawatafuta mafundi, wajuzi wa hii fani, Shamba langu la mahindi, limevamiwa na nyani, Wanakuja kwa makundi, tena wazi hadharani, Mkulima nina tabu, shamba kavamia nyani.
Sio kwamba sililindi, jamani nieleweni, Nimewategea gundi, wakija wanase chini, Cha ajabu hawagandi, sijui ati kwanini, Mkulima nina tabu, shamba kavamia nyani.
Nipendalo silitendi, moyo hauna amani, Hata…
View On WordPress


















