*YALIYOJIRI LEO AGOSTI 23, 2017 KATIKA MKUTANO KATI YA MKURUGENZI WA IDARA YA HABARI (MAELEZO) NA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI DKT. HASSAN ABBASI NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU KUANZA KWA ZOEZI LA UTOAJI WA LESENI ZA MACHAPISHO* #Dkt. Abbasi amewashkuru watanzania kwa kumuombea na kumfariji kipindi cha msiba wa mama yake mzazi. #Dkt. Abbasi amemshkuru Rais wa JMT, Dkt. Magufuli kwa kumteua kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali. Ameahidi kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi na uzalendo mkubwa. Amesema leo amewaita wanahabari kueleza maendeleo katika utekelezaji wa sheria mpya ya habari hasa vifungu vinavyotaka machapisho yote ya Serikali au Taasisi binafsi lazima yasajiliwe upya kwa kupewa leseni - Dkt. Abbasi. #Kuanzia leo hadi Oktoba 15, 2017 magazeti yote yahakikishe yanakuja kusajiliwa upya - Dkt. Abbasi. #Baada ya Oktoba 15, 2017 hakuna atakayeruhusiwa kuchapisha chapisho lolote bila usajili - Dkt. Abbasi. #Mfumo mpya wa utoaji leseni ni muendelezo wa azma yetu ya kuifanya tasnia ya habari kuwa taaluma- Dkt. Abbasi. #Mfumo mpya wa utoaji wa leseni ni maendeleo ya utekelezaji wa Sheria ya Huduma za Habari - Dkt. Abbasi. #Taratibu zote za upatikanaji wa leseni zimewekwa katika tovuti yetu www.maelezo.go.tz - Dkt. Abbasi. #Kigezo cha cheti cha usajili wa Kampuni hakitohusisha Taasisi za Serikali na badala yake watatakiwa kuwasilisha barua kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Taasisi - Dkt. Abbasi. #Fomu za maombi, akaunti ya kulipia na orodha za nyaraka zinazohitajika vinapatikana pia katika ofisi za MAELEZO za Dar es Salaam na Dodoma - Dkt. Abbasi. #Mawasiliano kwa ajili ya ufafanuzi kuhusu utaratibu wa usajili ni 0622664606 na 0717312417 au kupitia [email protected] - Dkt. Abbasi. #Mfumo wa utoaji leseni za machapisho umerahisishwa hivyo ndani ya siku 3 leseni itakua tayari imeshatoka - Dkt. Abbasi. #Leseni hizo zitahuishwa kila mwaka kwa mujibu wa kanuni zilizopo katika Sheria ya Huduma za Habari - Dkt. Abbasi. #Sheria mpya ya Huduma za Habari imeiweka taaluma ya habari kuwa katika mfumo wa kitaasisi - Dkt. Abbasi. *IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI (MAELEZO)*














