Mtu anaweza kuchanganyikiwa lakini akasema jambo fulani la hekima, akiongozwa na yule aliyemuumba; kwa sababu, katika macho ya Mungu, hakuna aliye chini au juu ya mwingine. Wote tuko sawa! Usimdharau mjinga, mpumbavu, mwendawazimu, au yule unayedhani anastahili kudharauliwa. Mwendawazimu anaweza kuzungumza jambo la maana, kwa maana ya kuongozwa na Mungu, hata yule anayemsikiliza au wale wanaomsikiliza akashangaa au wakashangaa. Siri ya mafanikio ni kutomdharau mtu yeyote, kwani kila mtu ana thamani sawa mbele ya Mungu. Mbele ya Mungu kila mtu ana nafasi sawa ya kuusifu uumbaji wa Mungu, kuutukuza na kuuheshimu pia. Hivyo ni vema tukaheshimiana, bila kujali hali zetu za kiafya au vinginevyo, hasa kwa kutilia maanani yale tunayoyazungumza kila siku, kwani kila mtu anaongozwa na Mungu huyohuyo aliyemuumba kila mtu anapozungumza. Kumbuka kuwa Shetani huwa anaingilia tu uongozi wa Mwenyezi Mungu kwetu, lakini hasa anayetuongoza ni Mwenyezi Mungu mwenyewe. Jambo la hekima linaloweza kunenwa na mjinga, mpumbavu, mwendawazimu, au yule unayedhani hastahili kuheshimiwa, linaweza kuwa la manufaa sana katika maisha yako. Hivyo, heshimu mtu awaye yote. -Enock Maregesi, mwandishi wa Kolonia Santita #heshima #respect #mwendawazimu #madman #mentallyunbalanced https://www.instagram.com/p/Bz6kSZOnpLs/?igshid=1fwwkiq1vn6j7









