#TRT: Ndege za Turkish Airlines kuongeza safari zake kuelekea Urusi Shirika la Ndege la Turkish Airlines linatarajia kuongeza safari zake kuelekea Urusi ifikapo mwaka 2018. Kwa mujibu wa habari,kwa kawaida ndege hizo hufanya safari mara nne ndani ya wiki moja kuelekea Urusi lakini sasa inatarajia kufanya safari za ndege nne kwa siku moja ifikapo mwaka 2018.











