Wengine Wanitamani!
Usinidharau kwa kunitazama tu. Unavyoniona kama sifai, wapo wengine wanaoujua wema wangu. Ni kwako sina la wema, wengine wanitamani!
Wanibeza kwa hujuma, bila la kunithamini, Mara kwa zako tuhuma, za kuonesha sifani, Kejeli zinaandama, kunifanza niwe duni, Ni kwako sina la wema, wengine wanitamani! Sikosi la taadhima, kwa hilo ulithamini, Si kwa mabaya kuvuma, siseme zuri sinani, Ola mambo kwa hikima, ulipate la kughani, Ni kwako sina la wema, wengine wanitamani! Kusaili utakwama, uwe na la walakini, Kilele chako hatima,…
View On WordPress











