Well done @SteveNyerere 👏🏽👏🏽 Ivi ni kwanini watanzania tunaona kama mtu kujua English ndio kushinda maisha?? English au Kiingereza ni lugha tu kama ilivo kiswahili, Kichaga, Kisukuma, Kichina, Kiganda n.k. China, Germany, France ni moja ya nchi tajiri duniani lakini hawaongei Kingereza, hata viongozi wao wa serikalini lugha ya Kingereza haiwahusu na wala haiwasumbui. Ma celebrity wao ndio kabisaaa. Sasa kwanini Sisi tumekua tunawanyooshea vidole wa-Tanzania ambao hawaongei Kingereza? Tena wengine wanajaribu halafu tunawacheka🤷🏽♀️ Embu tuweni wakweli, mtanzania wa kawaida aliekwenda shule ya kawaida (Achana na Ma-International School) Je Kiingereza anajifunzia wapi???? Halafu naomba mnitajie viongozi wazuri serikalini au Matajiri TZ waliotoka shule za International School? Inamaana kujua Kiingereza sio Big deal. Embu tuanze kuwaheshimu wale wanaodhubutu kuongea lugha za watu, hata ikiwa broken kiasi gani, tuwe tunawapa support na sio kuwacheka, KUJUA KINGEREZA SIO UJANJA. Nitakua na Kipindi Kwenye TV ya hapa Uingereza ambacho kitakua ni cha Kiswahili... Kitakua kwenye SKY 175 Kila Jumamosi saa MOJA JIONI ambayo itakua saa TATU Usiku Kwa muda wa Kitanzania. Tutakua pia LIVE online Hivyo utaweza kutuangalia popote pale ulipo duniani. Lengo la hiki kipindi ni kuitangaza Lugha ya KISWAHILI. Watanzania wengi wanafanya vizuri sana kwenye biashara zao huko Tanzania na nchi nyingine mbali mbali, lakini hawapati nafasi ya kuonekana ulaya kwasababu tu hatuzungumzi kiingereza.. NO.. NO. Hii Itakupa nafasi yako wewe Mtanzania Kuonekana kwenye SKY TV.. ambayo ni moja ya biggest sitellite duniani. Nitatumia hii platform kukikuza KISWAHILI, na Pia kuwaletea Watanzania wanaokaa Ulaya fursa zilizopo Tanzania: Kazi yangu kubwa itakua kukupa nafasi wewe Msanii, Muigizaji, Mfanya biashara au muekezaji nafasi yakuonekana dunia nzima. Hiki kitakua nikipindi cha Watanzania WOTE popote pale mlipo. Wewe kama Mtanzania unayo nafasi yakuonekana kwenye SKY TV kwakupitia #TheSporahShow #YaKiswahili #SKY175 Huu ndio Muda wa kuitangaza TANZANIA MPYA, bila kusahau MBUGA zetu za Wanyama, Mt. Kilimanjaro, Our Beautiful Zanzibar na Chakula chetu kitamuuuuu😋 #ComingSoon