Vitabu vilivyonipa miongozo kuhusu jinsi ya kukabiliana na changamoto za maisha. Ni rahisi sana kuona mafanikio ya watu. Ni rahisi sana kushangilia na na kuhukumu kuhusu maisha ya watu. Ni rahisi mno kutoa mtizamo wa maisha ya watu. Ni rahisi sana kufikiri waliofanikiwa wanashangilia mafanikio yao. Ni rahisi sana kuwafikiria kuwa maisha yao ni mteremko, mepesi, wana hela, hawana shida wala changamoto. Vitabu hivi vimenifanya nitafakari sana kauli ya βdonβt judge a book by its coverβ! Maisha na matukio wanauopitia watu tunaoona wamefanikiwa, yana changamoto nyingi zaidi kuliko hata mtu mwenye maisha ya kawaida. Hakuna hata mmoja aliyekuwa na maisha laini kama tunavyoamini kirahisi. Sio wote tunaweza kuandika vitabu kuhusu maisha yetu ili watu wasome na kujifunza. Lakini kwa vitabu hivi, nikiri tu kuwa nimehamasika kumaliza nilichokuwa natamani nifanye. #mylifemypurpose #njelukasaka #icanimustiwill #upakotokakuzimu #mimimwanakijiji #donttalktothemedia #bookreaders #booksof2019 #2019books https://www.instagram.com/p/B5w2yfVHQ2VE43NowaYh3SLf8TDnPkQvcxc5gs0/?igshid=hqu7xtxw0xvg












