Taasisi ya Uongozi Institute, iliyoandaa tawasifu ya Maisha Yangu, Kusudio Langu ya Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, inasema kuwa tawasifu hiyo imegharimu shilingi za Kitanzania milioni 230. Imetoa mfano wa tawasifu za Mheshimiwa Barack Obama, rais mstaafu wa Marekani, na mkewe Michelle Obama, kwamba tawasifu zao ziligharimu dola za Kimarekani milioni 60; hivyo shilingi milioni 230 si kitu kulinganisha na dola milioni 60 za Obama na mkewe. Swali langu kwa taasisi ya Uongozi Institute: Gharama hizi za kitabu cha Mheshimiwa Mkapa ni za maandalizi tu ya kitabu au ni za maandalizi pamoja na malipo ya awali ya mrabaha wa kitabu chenyewe? Mimi kama mwandishi ningependa kujua kwa nini kitabu kigharimu fedha nyingi kiasi hicho kuandaa. Huko nchini Amerika mwandishi wa nje au "ghostwriter" anaweza kutoza hata dola 100,000 kuandika kitabu kwa niaba ya mtu mwingine, mbali na gharama za uhariri na mambo mengine ya maandalizi ya vitabu. Je, tawasifu hii ya Mheshimiwa Mkapa imeandikwa na Uongozi Institute au Mkapa mwenyewe au mtu mwingine yeyote yule? - Dola za Kimarekani milioni 65 za tawasifu za Obama na mkewe ni fedha walizolipwa kama malipo ya awali ya mirabaha ya vitabu vyao, wala si fedha za maandalizi ya vitabu hivyo. Uongozi Institute tafadhali sana tupeni mchanganuo wa shilingi milioni 230 za gharama ya tawasifu ya rais wetu Benjamin Mkapa, ili nasi tujifunze kuanzia hapo. - -Enock Maregesi, mwandishi wa Kolonia Santita #uongoziinstitute #benjaminwilliammkapa #mylifemypurpose https://www.instagram.com/p/B4123WGnfkb/?igshid=1p757ahcfrnjs