Je, unamjua Mungu? Huyu ndiye Mungu: Mungu ni mkamilifu milele. Anaishi katika ukamilifu wa milele. Hivyo, kabla ya uumbaji, aliishi katika ukamilifu, baada ya uumbaji, ataishi katika ukamilifu. Ukiichunguza sana hii kauli utajua Mungu ni nani. Mungu ni Muumbaji, aliyekuwapo, aliyepo, na atakayekuwapo. Hapa duniani kuna watu wawili tu: Mungu na wewe! Wengine wote, vingine vyote, wako au viko kisogoni mwako. Nje ya macho yako kuna Nuru. Nuru hiyo ndiye Mungu. Wengine wote, vingine vyote, ni akisi ya taswira ambazo ziko ndani yako; ambazo unatakiwa kuziona nje ili uone umekosea sehemu gani, kusudi uweze kurekebisha dunia yako ya ndani. Wale wanasiasa wanaotuambia kila siku kuwa tulete mabadiliko duniani wanajisumbua iwapo hawatatuambia tulete mabadiliko ndani ya dunia zetu za ndani kwanza. Ukibadilisha dunia yako ya ndani, utabadilisha dunia yako ya nje bila matatizo yoyote. Yesu ni Mfalme wa wafalme, kwa sababu baada ya muda fulani atarudisha ufalme kwa Baba yake. Mungu ni Mfalme wa milele asiyeweza kuonekana wala asiyeweza kufa, 1 Timotheo 1:17, na haonekani kwa faida yetu wenyewe. Kwa nini? Kama Mungu yupo, yuko wapi? Kwa nini asijioneshe ili nasi tumwone? Kama alituumba, kwa nini hatuonani naye uso kwa uso? Kwani tatizo ni nini? Faida ya yeye kutojionesha kwetu ni nini? Mungu hawezi kujionesha kwetu kwa kuwa asili yetu ya ubinafsi itasababisha mtafaruku mkubwa, na matatizo makubwa, dunia nzima. Kila mtu duniani kote atamng’ang’ania, atamtamani sana, na hakuna la maana litakalofanyika. Fikiria tu kuwa Mungu ameonekana Tanzania na ameanzisha kanisa na watu wote duniani kote wameamini hivyo. Kila mtu duniani kote atapenda kwenda kwenye kanisa hilo kwa minajili tu ya kuonana na Mungu. Huo ndiyo mtafaruku ninaouongelea. Aidha, Mungu akijionesha kwetu itakuwa kinyume cha kusudi la maisha; kwani kusudi la maisha ni kuishi naye mbinguni kwa furaha ya milele, na hatutaweza kuishi naye mbinguni iwapo tuliishi naye duniani. Soma zaidi hapa: https://bit.ly/MwenyeziMungu #mungu #god #muumba #creator #ulimwengu #universe https://www.instagram.com/p/BykB1mHB6Hq/?igshid=1k7pl9glcptk