Luka 6:30 inasema, "Mpe kila akuombaye, na akunyang'anyaye vitu vyako, usitake akurudishie." Saidia hata watu wawili usiowajua kila mwezi katika maisha yako. Unaweza kusaidia mtu mmoja mmoja, au unaweza kufanya hivyo kupitia vituo vya kusaidia watu. Mtu akikuomba msaada na ukawa na mashaka naye mpe Mungu msaada huo amsaidie. Lakini, utampaje Mungu msaada ili amsaidie mtu? Kabla hujatoa msaada kwa mtu uombee kwanza kimoyomoyo msaada huo ndipo uutoe. Kwa kufanya hivyo umemsaidia Mungu. Katika kupata, tunaishi. Katika kutoa, tunapokea, tunatengeneza maisha. Sisi wote ni mali ya Mungu. Sisi wote ni watunzaji wa mali ya Mungu. #enockmaregesi #luke630 #charity #msaada #help #watotowamungu #childrenofgod https://www.instagram.com/p/Bq4SHSDnHRg/?utm_source=ig_tumblr_share&igshid=8sujnisbpk1i












